13 Oktoba 2025 - 16:41
Maulid Adhimu ya Mtume (s.a.w.w) Temeke Mwisho - Dar-es-salaam kuvutia wageni wa kitaifa na Kimataifa - Maandalizi yakamilika kwa Kiwango cha Juu

Dr. Alhad Mussa Salum ametoa wito kwa Waumini kuhudhuria kwa wingi, akisisitiza umuhimu wa kumuadhimisha Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa upendo na amani.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Hafla adhimu ya Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) imepangwa kufanyika Ijumaa, tarehe 17 Oktoba 2025, baada ya Swala ya Isha, katika Masjid Majmuuat Al-Islaamiyyat – Temeke Mwisho, jijini Dar es Salaam.

Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum, Imam Mkuu wa Msikiti huo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), amesema maandalizi yamekamilika na wageni mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi wamethibitisha kushiriki.

Miongoni mwao ni viongozi wa Kiislamu, Maulamaa kutoka Zanzibar na Afrika Mashariki, Masharifu, Masheikh wa Mikoa, pamoja na viongozi wa Serikali na Mabalozi.

Dr. Alhad Mussa Salum ametoa wito kwa Waumini kuhudhuria kwa wingi, akisisitiza umuhimu wa kumuadhimisha Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa upendo na amani.

Hafla hii inatarajiwa kuwa miongoni mwa maadhimisho makubwa zaidi jijini Dar es Salaam kwa mwaka huu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha